KOCHA mpya wa klabu za TMK United, Kennedy Mwaisabula amekipangua kikosi chote cha timu hiyo aliyoirithi toka kwa Fred Felix Minziro na kuanza mipango ya kuisuka upya kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara itakayofanyika Septemba mwaka huu.
Akizungumza na Full Mswano, Mwaisabula aliyewahi kuzinoa timu za Yanga, Bandari-Mtwara na Twiga Sports, alisema ameamua kukifumua kikosi hicho kwa lengo la kuhakikisha TMK Utd inapanda Ligi Kuu msimu wa 2011-2012.
Mwaisabula alisema ameweza kubaini kuwa katika kikosi kilichoshindwa kufuzu ligi kuu msimu huu kilikuwa kimejaa wachezaji wengi wazee na waliocheza kwa muda mrefu ligi kuu na hivyo kukosa mbinu za kiuchezaji.
"Nakipangua kikosi baada ya kubaini waliokuwepo kwa sasa wengi wana umri mkubwa au kucheza kwa muda mrefu kwenye ligi na hivyo nitatafuta chipukizi ambao naamini watanisaidia na kuitumikia TMK kwa muda mrefu," alisema Mwaisabula.
Mwaisabula, alisema kutokana na mipango yake ya kuunda kikosi kipya, amewaalika wachezaji vijana na wenye uwezo wa kisoka kujitokeza kufanyiwa majaribio kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyoanza tangu siku ya Jumanne kwenye viwanja vya Sigara, Chang'ombe.
Mwaisabula alisema mbali na kuwaomba wachezaji chipukizi kujitokea uwanja wa TCC, pia mwenyewe atakuwa akiifuatilia michuano ya Copa Coca Cola kusaka wengine.
Baadhi ya wachezaji walioichezea TMK msimu uliopita na kuzidiwa ujanja na timu za Ruvu Shooting Stars, Kelvin Mhagama na wakali wengine waliowahi kzuichezea Simba na Yanga.
No comments:
Post a Comment