Tuesday, July 6, 2010

Mr Ebbo asita kuingiza albamu sokoni, kisa...!


Mr. Ebbo asita kuweka albamu sokoni


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, 'Mr.Ebbo' amesema amesita kuingiza sokoni albamu yake

mpya ambayo hajaipa jina kwa madai albamu ya sita bado inaendelea kufanya vema kwa sasa.
Mr. Ebbo ambaye jina lake halisi ni Abel Loshilaa Motika, aliiambia Blog hii kwa njia ya simu toka

Tanga kuwa albamu yake ya sita iitwayo 'Watoto Wangu' bado ina mashabiki wengi.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, imeona ni vyema kuisitisha kwanza albamu ya saba ambayo

nayo amesema nyimbo zake zimakamilika na zimesharekodiwa katika studio yake ya Motika

Records.
"Nina albamu ya saba yenye nyimbo za Uzuri wa Kichina, Mama Rosa, Ninasaini, na Wazazi

Wangu ambazo kwa kweli ni moto wa kuotea mbali, lakini siipeleki sokoni kwa sasa," alisema Mr.

Ebbo.
Alisema kuwa nyimbo za albamu ya sita zinazoendelea kutesa sokoni ni 'Hajui Kupika',

'Kahamishwa', 'Kaka Hoza', 'Maisha Plastiki', 'Kunanuna', 'Mbado remix', 'Sikopi Tena', na 'Ulimi'.
Msanii huyo aliendelea kutaja nyimbo nyingine za albamu hiyo kuwa ni 'Bodaboda', 'Simu Feki',

'Tabia Mbaya' na 'Bado Naimba' ambazo alisema ameziachia nafasi ili ziendelee kumtangaza.
Mr. Ebbo aliyeibuka kwenye muziki wa kizazi kipya mwaka 2002, aliwahi kutamba na albamu yake

ya kwanza ya 'Fahari Yako' na nyingine kama 'Bado Ijasungumiswa', 'Kazi Gani', 'Alibamu',

'Kamongo' na ndipo alipoachia hiyo ya 'Watoto Wangu' inayoendelea kutamba sokoni.

No comments:

Post a Comment